Habari za Punde

Kaskazini Pemba kushirikiana na Wizara ya Elimu kukabiliana na changamotoza skuli ya Shumba Viamboni na Micheweni

Na Salmin Juma, Pemba

Serikali ya mkoa wa kaskazini Pemba imeahidi kushirikiana na wizara ya elimu na mafunzo ya amali mkoa huo kuzitafutia ufumbuzi baadhi ya changamoto zinazoikabili skuli ya sekondari ya Shumba Viamboni wilaya ya Micheweni .

Akizungumza katika mahafali ya nane (8) ya kidato cha nne kwa niaba ya mkuu wa mkoa  wa kaskazini pemba , katibu tawala mkoa huo Yussuf Mohammed Ali amesema serikali ya mkoa itafanya mazungumzo na baadhi ya wahisani ili kusaidia kuondoa changamoto hizo .

Aidha amewataka viongozi wa jimbo hilo mbunge na mwakilishi kuwa na karibu na karibu na skuli zilizomo ndani ya jimbo ili kuelewa changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi unao faa kwa maendeleo ya skuli hizo.

Akizungumzia tatizo la ukosefu wa huduma ya umeme katika ofisi ya mkuu , afisa elimu mkoa mohammed nassor salim ameaguza uongozi wa skuli hiyo kufanya tathmini na makadirio ya fedha na kuziwasilisha ofisini kwake kwa hatua za utekelezaji .

Mapema uongozi wa skuli hiyo umesema kuwa unakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa nyumba za walimu, maabara, maktaba pamoja na kompyuta  na printer.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.