Habari za Punde

Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi Azindua Rasmin Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi leo Dar.

Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizindua rasmi Kamisheni ya Tume ya Mipango na Matumizi ya Ardhi katika ukumbi wa Tume Jijini Dar es salaam leo.
Dr. Stephen Nindi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania akitoa utambulisho wakati wa uzinduzi wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi
Mwenyekiti wa Kamisheni Mstaafu Bw. Abubakar Rajabu akizungumzia hatua walizofikia wakati akiwa mwenyekiti mpaka walipofikia kabla ya kumaliza muda wake na kumpongeza hatua zinazoendelea kwa sasa katika Tume hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Fidelis Mutakyamilwa akitoa neno la Shukurani kwa Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada ya uzinduzi rasmi wa tume na kuleleza kuwa wanaanza kuyafanyia kutekeleza mara moja maelekezo waliyopewa na Mh. Lukuvi
Makamishna wateule, Pamoja na Menijimenti ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi wakiwa katika uzinduzi huo.
Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume pamoja na Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi
Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi,Mwenyekiti,Katibu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo
Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi

Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.