Habari za Punde

Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari ya Baraza la Wawakilishi ziarani Pemba

 MWAKILISHI wa Jimbo la Paje Jaku Hashim Ayoub ambae ni mjumbe wa Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari akisoma, moja kati ya mabango yanayotoa taarifa kwenye eneo la kihistoria la Mkamandume wilaya ya Chakechake Pemba, wakati wajumbe wa kamati hiyo ilipotembelea eneo hilo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 ENEO la kihistoria la Mkamandume Pujini wilaya ya Chakechake, likianza kupoteza uasili wake taratiibu, ambapo Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habar ya baraza la wawakilishi ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ali Suleiman Shihita, ilitembelea na kusikitishwa na hali iliopo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 KAIMU mkuu wa Idara ya Makumbusho ya Mambo ya Kale Pemba Salim Seif, akiwafahamisha jambo wajumbe wa Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari, kwenye eneo la kihistoria la Mkamandume Pujini wilaya ya Chakechake Pemba, wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo hilo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
  MKURUGENZI Mipango sera na utafiti wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Mahamoud Omar Hamad, akitoa ufafanuzi juu ya kuliimarisha eneo la kihistoria la Mkamandume Pujini wilaya ya Chakechake kwa Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari, wakati kama hiyo, ilipotembelea eneo hilo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 AFISA Mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Pemba Khatib Juma Mjaja, akijibu sualia la wajumbe wa Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari, kwenye eneo la kihistoria la Mkamandume Pujini wilaya ya Chakechake, wakati kamati hiyo, ilipotembelea eneo hilo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
  MWENYEKITI wa Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari Ali Suleiman Shihita, akiomba ufafanuzi, kuhusu kuachwa kuharibika kwa eneo la kihistoria la Mkamandume Pujini Wilaya ya Chakechake Pemba, wakati kamati hiyo ilipotemebele eneo hilo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WAJUMBE wa Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari, wakiongozwa na Mwenyekiti wake,  Ali Suleiman Shihita, wakitembelea eneo la kihistoria la Mkamandume Pujini wilaya ya Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WAJUMBE wa Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari, wakiongozwa na Mwenyekiti wake,  Ali Suleiman Shihita, wakitembelea eneo la kihistoria la Mkamandume Pujini wilaya ya Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WAJUMBE wa Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari, wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Ali Suleiman Shihita, wakielekea kupanda boti, ili kukikagua chumba cha chini ya bahari, kilichoko hoteli ya Manterif Makangale wilaya ya Micheweni Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MDHAMINI wa Kamisheni ya Utalii Pemba Suleiman Amour (mweye koti), akiwaonyesha mipaka wajumbe wa Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji, na Habari ya baraza la wawakilishi, eneo la Vuma wimbi Mkangale, wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo hilo, (Picha na Haji  Nassor, Pemba).    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.