Habari za Punde

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF),Watoa Msaada wa Komputa kwa Shule ya Sekondari Chalinze Mkoa wa Pwani.


Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, (UCSAF), Joseph Kilongola, (wakwanza kushoto-mbele), Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Mhandisi Peter Ulanga, (wakwanza kushoto-nyuma), wakishuhudia Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (anayeshughulikia sekta ya Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora, (mwenye tai nyekundu), Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete, (wakwanza kulia), Diwani wa Kata ya Bwilingu, Lucas Lufunga, (wane kulia), na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Edes P.Lukoa, wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya kopyuta zilizotolewa na UCSAF kwa shule ya Sekondari Chalinze mkoani Pwani.


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO wa Mawasiliano kwa wote, (UCSAF), umetoa msaada wa kompyuta 10 kwa Shule ya Sekondari Chalinze mkoani Pwani ikiwa ni moja ya jitihada za Mfuko huo kuwawezesha wananchi wa kada mbalimbali kupata fursa ya mawasiliano.
Akizungumza wakati wa makabidhiano rasmi ya msaada huo, shuleni hapo mwishoni mwa wiki, mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Joseph Kilongola alisema, mfuko ulipokea maombi kutoka shule hiyo ya uhitaji wa kompyuta ili kuwawezesha wanafunzi na jamii inayozunguka shule hiyo kupata fursa ya kujifunza teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta. 
"Ili kuwafundisha watoto wetu kupitia internet, ni vizuri shule iwe na kompyuta za kutosha, Mfuko ulikubali ombi la shule ili kuwapatia kompyuta 10  kuiwezesha maabara yao ya kompyuta kutumika kwa ufanisi zaidi, na ni matumaini yetu kuwa kompyuta hizi zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuwaelimisha wananfunzi na kuwawezesha walimu kuzitumia kama nyenzo ya kupata maarifa ya ziada kwa ajili ya kufundisha na hivyo kuboresha maendeleo ya wananfunzi na jamii inayotuzunguka." Alisema na kuongeza.
 Baadhi ya kompyuta zilizotolewa na Mfuko kwa shule hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCSAF), Joseph Kilongola 
"nimeelezwa na mheshimiwa Mwalimu Mkuu, kuwa jumuiya inayotuzunguka Chalinze sekondari inakuja kujifunza hapa wakati mwingine namna ya kutumia komyuta kwakweli hili ni jambo zuri na ndio malengo ya mfuko kuhakikisha jamii inafikiwa zaidi na huduma za mawasiliano." Alifafanua Mwenyekiti huyo wa bodi.
Mfuko wa mawasiliano kwa wote ni taasisi ya serikali ambayo jukumu lake kubwa ni kuhakikisha sehemu ambazo wananchi hawafikiwi vilivyo na huduma za mawasiliano kama vile simu kutoka mitandao mbalimbali, Mfuko uhakikishe unahamasisha makampuni hayo kufikisha huduma hiyo kwa wananchi. "Serikali baada ya kugundua makampuni ya kutoa huduma za mawasiliano hayavitiwi kuwekeza maeneo ya vijijini, kwa kuhofian kutopata faida, ikaanzisha mfuko huu mwaka 2006 ili ksehemu kama hizo zikitambuliwa, taratibu zifanyike kuwahamasisha hao wawekezaji waweze kwenda huko ili kuhakikisha huduma za mawasuikliano zinawafikia watanzania, na wachangiaji wakubwa wa Mfuko huu ni serikali na makampuni yote yanayotoa huduma za mawasikiano yanachangia Mfuko huo na wadao wanaotakia mema nchi yetu kama vile Benki ya Dunia huchangia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCSAF), Mhandisi Peter Ulanga, akizungumza wakati wa makabidhiano hayo
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, (anayeshughulikia mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora, ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwaasa wanafunzi kujifunza zaidi elimu ya kompyuta na sio kujifunza word, excel na access, kwa sasa mafunzo hayo hayatoshi, na hivyo aliwahimiza wanafunzi lkujifunza zaidi ya hapo na hususan kutengeneza nyenzo za kutumia kompyuta, (computer applications).

"Wenzetu huko nchi za nje ambako wametutangulia katika teknolojia hii ya mawasiliano ya kompyuta, tangu shule za vidudu watoto wanafundishwa jinsi ya kuandika programs, bila shaka sisi sote wenye simu za mikononi kwenye simu zetu tunazo nyenzo mbalimbali (applications),  tunazozi zitumia kupakua (dowload), vitu mbalimbali  kutoka Google play, kwa hivyo ni vema tukaanza kujiongeza ili kupata manufaa zaidi ya kompyuta." Alisema Profesa Kamuzora.

Mbunge wa chalinze, Ridhwani Kikwete, aliushukuru mfuko wa UCSAF kwa msaada huo kwani utasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa kompyuta shuleni hapo. "Naamini msaada huu utatusaidia sana kuhakikisha wananfunzi wetu wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kupitia internet lakini pia kujiongezea maarifa mbalimbali yatokanayo na kompyuta.

 Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete, (aliyesimama), akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea msaada wa kompyuta hizo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji wa UCSAF, Mhandisi Peter Ulanga, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Edes P.Lukoa.

 Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Joseph Kilongola, (kulia), akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Ulanga, wakijadiliana jambo
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora, (aliyesimama), akitoa hotuba yake

 Mbunge wa Chalinze, Rizwani Kikwete, (kulia), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora, wakati wakitembelea maabara ya kompyuta ya shule hiyo
 Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Kamuzora, Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete, Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Ulanga, na viongozi wengine wakitembelea maabara hiyo.
 Mkuu wa Huduma za Manunuzi wa UCSAF, John S.Munkondya, (kushoto), akiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Chalinze, Emmanuel Kahabi
 Mbunge Kikwete, akiteta jambo na Mhandisi Ulanga
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya kompyuta

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.