Habari za Punde

Waziri Aboud akagua ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi bonde la Koowe, Micheweni

 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe:Mohamed Aboud Mohamed akipata maelezo juu ya ujenzi wa tuta la kuzuwia maji Chumvi lenye urefu wa mita 1600, lililogharimu zaidi ya Milioni 300, kutoka kwa afisa umwagiliaji Pemba Mbarouk Ali Mgau, huko katika bonde la Koowe Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 TUTA la kuzuwia maji chumvi lenye urefu wa mita urefu wa mita 1600, likiwa limejengwa katika bonde la Koowe Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba, ambapo kwa sasa wananchi wameweza kurudi katika shughuli zao za kilimo baada ya kujengwa kwa tuta hilo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akizungumza jambo mara baada ya kupewa maelezo juu ya ujenzi wa tuta la kuzuwia maji Chumvi huko katika Bonde la Koowe shehia ya Wingwi Wilaya ya Micheweni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.