Habari za Punde

Waziri Hamad Awataka Watendaji wa Wizara yake Kubadilika Kiutendaji.

Na Salmin Juma. Pemba. 
Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid Muhammed,amewataka watendeji kupitia wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kwamba wanatakiwa wawe na kasi ya haraka katika utekelezaji wa makujumu yao ili maendeleo yafikiwe kwa haraka zaidi.

Amesema kufuatia ziara ya kuwatembelea wakulima na wafugaji ya siku tatu kisiwani Pemba amejifunza mengi sana ikiwemo la baadhi ya watendeji katika wizara hiyo kutowajibika ipasavyo.

Waziri Hamad ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Weni  wilaya ya wete mkoa wa Kaskazini Pemba alipokua akizungumza na waratibu wa miradi, wasimamizi wa mashamba ya karafuu pamoja na wataalam wa umwagiliaji wa wizara hiyo.

Akizungumza kwa hamasa waziri huyo ameonyesha kusikitishwa vikubwa kutokana na wakulima na wafugaji kisiwani Pemba kua, wapo tayari na wameshahamasishika katika harakati zao lakini bado watendaji kutoka serikalini wamelala na hatimae mpaka leo bado hakujawa na mafanikio ya kutosheleza katika sekta ya kilimo na ufugaji nchini.

Katika kutilia mkazo utendaji bora kwa wafanyakazi wa wizara hiyo ametoa agizo la kuwataka watendaji hao kwa kila mmoja kuandaa mpango maalum utakaonesha ametembelea wapi na amefanya nini na baadae atapitia daftari hilo kutazama kila mmoja na alichokifanya huku akisema kua atakaeonekana kuzembea hakunabudi kukaa pembeni.

Amesema afisa lazima aeleze kama amekwenda sehemu gani na mekuta shida gani inayomkabili mkulima baadae asaidie kutatua changamoto hiyo na si kuweka katika rikodi pekee na kama hatokua na vitendea kazi asisite kusema wizarani ili kwa pamoja walitafutie suluhisho hatimae mkulima awe katika mazingira salama na kipando chake.

Akiendelea kutilia mkazo kua maafisa wa wizara hiyo bado wapo nyuma kiutendeji amesema kua ziwani mkoa wa kusini Pemba kuna mfugaji amejiimarisha vizuri kwa kufuga kuku wa mayai lakini mabanda anayofugia yanaonekana hayapo kitaalamu na hiyo inadhihirisha wazi kua watendaji hawakutoa ushauri kwa mfugji huyo.

Aidha amesema kilio kikubwa kwa walimu na wafugaji ni kutokua na soko la uhakika huku akiwataka maafisa wa wizara kujikita zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya lishe bora ili wananchi watumie bidhaa na baadae kutapatikana soko la uhakika

“juzi kuna wafugaji wanasema hakuna soko la mayai, lakin ukitazama kwa undani kila mtu mmoja anatakiwa ale yai moja kwa siku, ikibigwa idadi ya mayai wanayoyazalisha hayatoshelezi kwa wananchi wote na hapo ndipo unapogundua ,kumbe tatizo ni wananchi tu kutojua lishe bora kama wanaelewa bado soko lipo, maafisa hili ni jukumu lenu”alisema Hamada Rashid.

Katika hatua nyengine waziri Hamad Rashid amesema kua utunzaji wa  mali za serikali kama vile mashamba na pikipiki si mzuri , yapo yaliyopotea kwa kufichwa kwa makusudi, hivyo ametoa agizo la  miezi mitatu tu kwa watendaji hao kuleta taarifa kamili juu ya mali hizo.

Kwa muda wa siku tatu tokea 05/11/2016 mpaka  07/11/2106  Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid ametelembelea baadhi ya wakulima,wafugaji na maeneo ya uwekezaji katika mokoa yote miwili ya Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.