Habari za Punde

Jopo la Makocha Zanzibar Lamchagua Kocha Bora wa Mwezi Disemba Ligu Kuu ya Zanzibar Abdulghani Msoma Kuwa Kocha Bora.

Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe Ali Salum akimkabidhi seti ya Trek Suit Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar kwa Mwezi wa Disemba 2016 Kocha wa Timu ya KVZ kocha Abdulghani Msoma kwa kuibuka mshindi kwa kinyanganyiro hicho. Hii ni zawadi ya Pili kutolewa na Jopo la Makocha Zanzibar kufuatilia michezo ya Ligu Kuu ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Amaan wakati wa mchezo wa mwisho wa raundi ya kwanza kati ya Kimbunga na KVZ, uliofanyika uwanja wa amaan. timu ya KVZ imeshinda mchezo huo.
Kocha Msoma akipokea zawadi yake iliotolewa na Jopo la Makocha Zanzibar, akikabidhi zawadi hiyo Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe. Ali Salum. 
Kocha msoma akisalimiana na Makocha wanaounda Jopo hilo baada ya kukabidhiwa zawadi yake hiyo.
Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe Ali Salum akimkabidhi virimbi Refarii Bora kwa Mwezi wa Disemba kwa uchezeshaji wake mzuri na kuchaguliwa na Jopo la Makocha kuwa Refaarii Bora kwa Mwezi huu wa Disemba 2016. 
Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe Ali Salum. akimkabidhi zawadi iliotolewa na Jopo la Makocha Zanzibar Mchezaji Bora wa Mwezi Disemba  mshambuliaji wa Timu ya Polisi Zanzibar viatu vyenye thamani ya shilingi 45,0000 /=

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.