6/recent/ticker-posts

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli Amuapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania (CDF) Pamoja na Viongozi Wengine Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Jenerali Juma Malewa kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Paul Meela kuwa Balozi nchini DRC Congo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Samuel Shelukindo kuwa Balozi nchini Ufaransa, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Nyakimura Muhoji kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvisha cheo Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Jenerali kabla ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kwenye Ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvisha cheo Meja Jenerali James Makibolwa  kuwa Luteni Jenerali kabla ya kumuapisha kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kwenye Ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya tukio la uapisho lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba fupi baada ya hafla ya kuapishwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo (hayupopichani) katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo (katikati waliokaa) Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza mara baada ya tukio la Uapisho wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania pamoja na  Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza masuala mbalimbali mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi pamoja viongozi wengine wa Jeshi na Mabalozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza masuala mbalimbali mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi pamoja viongozi wengine wa Jeshi na Mabalozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (wakwanza kushoto), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wapili kulia pamoja na Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (watatu kutoka kushoto), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wanne kutoka (kulia) , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (wakwanza kushoto), Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo(watatu kutoka kulia ), Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Luteni Jenerali James Mwakibolwa (wapili kutoka kushoto),  Kamishna Jenerali wa Magereza Juma Malewa(wapili kutoka kulia) pamoja na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma(wakwanza kulia) Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali Devis Mwamunyange (katikati) Mkuu wa Majeshi Mpya Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Dkt.Juma Ali Malewa (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa wateule hao leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi  (IGP) Ernest Mangu mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments