Habari za Punde

Serikali kujenga Bandari ya kisasa Wete

Na Mwandishi wetu

Naibu katibu mkuu  UVCCM  zanzibar Abdullighafari Idirisa  Juma amesema  serikali ina mpango  wa  kujenga  bandari mpya  ya kisasa  wete  ili kuinuwa shughuli  za  kiuchumi kwa wananchi.

Ameyasema hayo huko bandarini Wete  katika ziara yake    ya kuangalia  shughuli mbali mbali za maendeleo pamoja na  matawi ya ccm  ikiwa ni  miongoni  mwa utekelezaji wa  ilani ya chama cha mapindunzi..

Amesema kukamilika kwa bandari ya wete   kutatoa fursa kwa wananchi kisiwani pemba kuendeleza shughuli zao za biashara kwa uhakika .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Wete,Rashid  Hadidi  Rashid  amesema shughuli za uchumi  katika  wilaya hiyo  zinaimarika kutokana  na kuwepo  kwa miundombinu ya uhakika ikiwemo maji safi na salama barabara pamoja na umeme  jambo  ambalo linawafanya wananchi kujiimarisha  kiuchumi kwa miradi mbali mbali ya kimaendeleo. 

Nae Mkurugenzi wa bandari Pemba, Hamad Salim Hamad amesema tayari kumejitokeza mfanya  biashara  ambae  anataka kuwekeza katika bandari hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.