Habari za Punde

Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba,

Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia waathirika kisiwani Pemba, Zanzibar, Tanzania

Assalaamu Alaykum warahmatuLlaahi wabarakaatuh

Mwezi mtukufu wa Ramadhaan umekaribia. Kutokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha nchini Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla umeleta uharibifu mkubwa wa nyumba, miundo mbinu, mashamba na vipando.

Kuna ndugu zetu watakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula katika mwezi mtukufu wa Ramadhaan kutokana na maafa haya.

Jumuiya ya Al Iman ya Northamptonshire nchini Uingereza imeamua kuwasaidia waathirika wa maafa haya hasa kisiwani Pemba kwa kuanzisha “Kikapu cha Ramadhaan” (Ramadhaan Basket) ambapo ndani yake mtakuwa na vitu muhimu kama mchele, unga wa ngano, sukari, mafuta ya kupikia na majani ya chai na kadhalika 

Kwa Pauni  £25.00 tu unaweza kujipatia kikapu chako na mchango wako angalau kuwapunguzia ukali wa maisha ndugu zetu walioathirika na maafa hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhaan.

Tunakuomba kwa moyo mkunjufu, andaa kikapu chako sasa na atakulipa kwa mchango wako kwa kuchangia Pauni 25.00 tu kwa kikapu kimoja. (unaweza kuongeza vikapu zaidi ukihitajia) 

Al Iman Society of Northamptonshire ni Jumuiya iliyosajiliwa kama Jumuiya ya khiari yenye makaazi yake Northampton ikiwa na namba ya usajili  1117020 

Kutuma mchango wako, Lloyds Bank sort code 309609  Account 03539228
Tumia reference: ‘Ramadhaan Basket’

Kama utachangia kwa njia ya cheki hakikisha cheki imeandikwa na kulipwa kwa  Al – Iman Society of Northamptonshire. Na upande wa nyuma iandikwe:  ‘Ramadhaan basket’

Au unaweza kutuletea kwenye Msikiti wetu: Northampton Mosque & Islamic Centre, Clare Street, Northampton NN1 3JF England

Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi wasiliana na Amiyr wa Jumuiya: Ustaadh Abdulrazak +44 7951816208 au email iman@al-iman.co.uk

Baaraka Llaahu fiykum

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.