Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Awasili Zanzibar Akitokea Ziarani Nchi Jordan.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na baadhi ya Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Serikali mara alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume akitokea Nchini Jordan kushiriki Mkutanowa Jukwaa la Dunia la Uchumi akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzanmia Dr. John Pombe Magufuli.
Balozi Seif  Kushoto akibadilishana Mawazo na Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika chumba cha Watu Mashuhuri {VIP} Kongwe.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewasili Zanzibar akitokea Mjini Amman Nchini Jordan kuhudhuria Jukwaa la Dunia la Uchumi World Economy Forum - WCF} la Siku Tatu litakalohudhuriwa na zaidi ya Wajumbe 2,000 kutoka Nchi 58 Duniani.

Balozi Seif  alimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa hilo la Kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika lililoshirikisha Viongozi Wakuu wa Nchi, Wafanyabiashara,wamiliki wa Makampunni ya Kimataifa, Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia, Mashirikia ya Kimataifa, Wana Habari pamoja naVijana wapatao 2,000.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alipokewa na  baadhi ya Mawaziri, Watendaji Wakuu  wa Serikali pamoja naViongozi wa Kisiasa. 

Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif aliongozana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar  Balozi Amina Salum Ali, pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.

Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif na Ujumbe wake alishiriki Washa ya Utalii iliyojikita zaidi katika masuala ya Kujenga Uchumi kwa Mataifa yaMashariki ya Kati na yale ya Kanda ya Afrika  ili kuona njia gani
zinaweza kutoa fursa za ajira kwa Vijana kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa

Mkutano huo wa Jukwaa la Uchumi Duniani ulifunguliwa na Kiongozi wa Jordan Mfalme wa Pili Abdullah  Bin Al-Hussein kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa King Hussein Bin Talal katika Bahari Nyeusi.

Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Fforum - WCF} limeasisiwa Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake  Profesa Klaus Schwab huko Davos, Switzerland.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.