Habari za Punde

Mkutano Mkuu Wa Umoja wa Watanzania Ujerumani 2017 watingisha Essen

Umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V watingisha jiji la Essen nchini Ujerumani baada ya kufanya mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba  ulioandamana na sherehe za ushindi wa viongozi wapya. Hapo jijini Essen katika ukumbi wa Bob's Cafe, watanzania zaidi ya 75 ambao wanaishi nchini humo walihudhuria mkutano huo ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wao, katika safu ya uongozi mpya Mhe Mfundo Peter Mfundo alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa umoja huo baada ya kukosa mpinzani. Makamo mwenyekiti mpya ni Mhe Salim Malumbo Jr. Katibu mkuu ni Julieth Myn, muweka Hazina ni Bi Nashe Mvungi, Mkaguzi wa mahesabu  namba 1 ni Mhe Bi Jovither Mushashu, Mkaguzi wa mahesabu namba 2 ni mhe Bi. Lilian Sorogo. Mjumbe namba Moja ni  Mhe Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja na Mjumbe namba 2 ni Mhe Vanessa Lymo. pamoja na mengi yalioongelewa kwenye mkutano huo azma ya  umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V ni kuwaendeleza watanzaniawanaoishi hapa ujerumani na hata kuwaletea maendeleo watanzania wanaoisho Tanzania, umoja ni Nguvu na utengano ni Udhaifu.

 Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Wanaoishi Nchi Ujerumani Ndg Peter Mfundo akizungumza wakati wa mkutano huo mkuu wa Umoja wa Wanatanzania Ujerumani.anzania waishio Ujerumani wakifur ... o mkuu wao mjini Essen,Ujerumani
 Watanzania wanaoishi Ujermani wakiwamo mkuu mjini Essen,Ujermani
 Mambo ya mnuso mnuso wa vyakula vya kinyumbani
Mhe.Mfundo,mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Ujerumani(UTU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.