Habari za Punde

DC Chake: Hakuna Mwananchi Atakaekosa Msaada

Na Salama Nassor, Pemba
MKUU wa wilaya ya ChakeChake, Salama Mbarouk Khatib, alisema hakuna mwananchi yeyote aliepata athari ya mvua zilizopita, atakaekosa msaada, kila wafadhili pale wanapojitokeza kwani yeye ndie mwenye jukumu la Wilaya yake.

Alisema hayo kwa nyakati tofauti, wakati  akifanya zoezi la ugawaji wa fedha kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu kwa waathirika hao, msaada   ambao uliotolewa na jumuia ya wafanyabishara wa mafuta ya reja reja kutoka Tanzania bara (TAPSOA).

Alieleza wananchi wasiwe na hofu, maana Serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wake, sambamba na kuwatafutia wafadhili wengine, ili kuwapa misaada kwa lengo la kuwafariji.

Mkuu huyu wa Wilaya ,alisema ingawa tayari misaada kadhaa imeshatolewa na kuwafikia walengwa, lakini kutokana na athari waliopata, wataendelea kuwatafutia wafadhili wengine.

“Nawahakikishieni wananchi  nyote wa Wilaya yangu mliopata athari za mvua nipo nanyi bega kwa bega na sitofanya upendeleo na kwani mie ni kiongozi wa wote na sio wa watu maalumu”,alisema.

Kwa upande wake, mweka hazina wa jumuia hiyo, Joh’n Muzalemwa Kiongozi, alisema lengo la kufika Kisiwa cha Pemba ni kutoa msaada baada ya kuguswa mno na athari za mvua zilizowakumba wananchi, hasa wa wilaya ya chakechake.

Alisema ingawa kima cha Tsh,100,000/=  (laki moja)  kwa ajili waathirika hao ni kigodo, lakini kitawasaidia kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya eid-elftri.

“Nilikuwa nasikia kama mlipata maafa lakini nimejionea mwenyewe na nimepata masikitiko makubwa lakini nawahakikishieni nitarudi tena na nitapigia harambee  kwa jumuiya nyengine ”,alisema.

Nao waathirika wa  mvua waliipongeza jumuia hiyo, pamoja na uongozi wa wilaya, kwa juhudi zao wanazozichukuwa , hali iliosababisha kupatiwa misaada mbali mbali , ikiwemo na huu ambao umewafikia wakati mwafaka.

Jumla ya Tshilingi milion 10, zimetumika kuwasaidia waathrika wa mvua Wilaya ya Chake Chake, na tayari huo ni msaada wa tano kwao, ukiwemo uliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dokta  Ali Mohamed Shein na taasisi mbali za kijamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.