Habari za Punde

Makocha watakiwa kujiunga na ZAFCA, ni baada ya ZFA kupata uanachama wa CAF

Katibu Mkuu msaidizi wa ZAFCA , Mustafa Hassan

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Makocha wa soka Visiwani Zanzibar wametakiwa kwenda kujiunga na Chama cha Makocha “ZAFCA” ili kuzidi kuendeleza taaluma yao ya ukocha kwa kupata fursa mbali mbali zikiwemo kozi za makocha.

Kauli hiyo ameitoa katibu msaidizi wa ZAFCA Mustafa Hassan wakati anazungumza na Mtandao huu kwa kuwataka makocha waende wakajiunge na chama chao.

Amesema baada ya Zanzibar kupata uanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” wamepokea mabadiliko na wametakiwa makocha wote wajiunge na chama chao ili watambuliwe na ZFA.

“Nawaomba makocha wenzangu waje kujiunga na ZAFCA, mana huko tunakokwenda ni kugumu mno, baada ya ZFA kuwa mwanachama wa CAF, tumetakiwa makocha wote wajinge na chama chao ili watambuliwe na ZFA na hapo ndipo utapata fursa ya kusoma kozi mbali mbali za makocha”. Alisema Mustafa.

Chama hicho cha makocha Zanzibar wanakutana kila siku ya Jumamosi katika darasa la Shule ya Sekondari ya Haile Selassie kuanzia saa 4:00 za asubuhi hadi saa 6:30 za mchana, hivyo kwa kocha yeyote anaetaka kujiunga na chama hicho afike hapo Haile kwa siku hiyo au amtafute kocha Nassor Salum wa Polisi au kocha Ibrahim Makeresa kwa kupatiwa fomu ya kujinga na uanachama ambayo inauzwa shilingi elfu mbili tu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.