Habari za Punde

Kikosi Cha Umisseta Kanda ya Unguja Kitakachokwenda Mkoani Mwaza Kimepatikana.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kocha msaidizi wa timu ya soka Kanda ya Unguja Abdul wahab Dau “Mwalimu Dau” ametangaza kikosi kipya wachezaji 21 cha timu hiyo ambacho kinatarajiwa kwenda Butimba Jijini Mwanza  katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)yanayotarajiwa kuanza  June 6, 2017.

Kikosi hicho kinatarajia kuondoka Visiwani Zanzibar siku ya Jumamosi ya June 3, 2017.
WALINDA MLANGO
Aley Ali Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu)
WALINZI
Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious), Abubakar Khamis (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba),  Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya.

VIUNGO
Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji Suleiman (JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni) na Eliyasa Suleiman (K-pura).

WASHAMBULIAJI
Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu), Walid Abdi “Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali Omar (Mwera).

Mashindano ya UMISSETA yanayotarajiwa kuanza June 6, 2017 huko Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu Zanzibar itashiriki kanda mbili tofauti, yani Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.