Habari za Punde

RC Ayoub alipofanya ziara ya ghafla na kukutana na vijana walioathirika na madawa ya Kulevya Kundemba

 Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Mhe Ayoub Mahmoud akisalimiana na mmoja wakaazi wa mtaa wa Kundemba katika wilaya ya mjini Zanzibar alipofanya ziara ya ghafla na klubndilishana nao mawazo katika mambo muhimu hivi karibuni. Ikumbukwe mtaa wa Kundemba ni Moja kati ya maeneo yaliyokithiri kwa matumizi ya madawa ya kulevya katika Mkoa wa Mjini Magharibi
  Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Mhe Ayoub Mahmoud akiwasikiliza makini vijana wa Kundemba wakitoa yao ya moyoni hii ni moja katika kuendeleza mradi wa MIMI NA WEWE wa kuondoa tatizo la madaqwa ya kulevya mkoani humo

  Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Mhe Ayoub Mahmoud akiwa sambamba na Mkuu wa wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas wakiendela kuwasikiliza vijana wa Kundemba ambao wengi wameathirika na madawa ya kulevya

Vijana wa Kundemba wakiwa hawaamini kilichotokea kwa kutembelewa na Mkuu wa Mkoa pamoja na Wilaya wakati mara nyinghi hukumbana na Polisi 

Kama umeguswa na ungependa kushiriki kuchangia Kampeni ya MIMI na WEWE unaweza kufika katika ofisi ya Mkuu wa mkoa Vuga na kuwasilisha Mchango wako

MIMI NA WEWE TUOKOE VIJANA WETU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.