Habari za Punde

Semina Elekezi Kwa Masheha Wapya wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Mwanasheria wa Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja  Miza Herman Mgisa  akiwasilisha Mada Wajibu wa Sheria Kwa Masheha wakati wa semina elekezi ya Masheha hao baada ya kuapishwa na kujuwa majukumu yao katika kazi hiyo, semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani kikwajuni Zanzibar
Waheshimiwa Masheha wakiwa makini wakifuatilia Semina hiyo wakati ikiwasilishwa Mada ya Sheria ya Utendaji wa Kazi yao katika Jamii wakati wa semina hiyo ya Siku tatu ilioandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika ukumbi wa zamabi wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.Sheha akichangia Mada wakati wa Semina hiyo elekezi kwa ajili ya Utendaji wa kazi zao za kila Siku.
Sheha wa Shehia ya Mchangani Unguja akichangia Mada iliowasilishwa na Mwanasheria wa Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja  Miza Herman Mgisa  wakati wa semina elekezi ya Masheha hao baada ya kuapishwa na kujuwa majukumu yao katika kazi hiyo, semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani kikwajuni Zanzibar
Baadhi ya Masheha Wapya wakifuatilia Semina Elekezi ilioandaliwa na Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani kikwajuni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.