Habari za Punde

Bushuri Kwenda Kuwasaidia Muembeladu

Na: Abubakar Khatib Kisandu, 
Kocha wa zamani wa Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushiri Mahmoud (Bush) amejitolea kwenda kuisadia timu ya Muembeladu inayoshiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.

Bushiri ambae kwasasa amerejea kwa muda Visiwani Zanzibar kufuatia mwanzoni mwa msimu huu kutoendelea tena kuifundisha Mwadui, sasa ataenda kuisaidia Muembeladu ambao wamemuomba kwenda kuisadia timu hiyo.

Akithibitisha kwenda kuwasaidia Muembeladu Bushiri amesema Muembeladu wamemfata kuwasaidia na yeye hakufanya hiyana kakubali kwenda kuwasaidia huku pia akisubiria mipango yake mengine ya kurejea Tanzania bara.

"Wamenifuata Uongozi wa Muembeladu nikawasaidie, sasa na mimi nimeona nkawasaidie ila nimeshawaambia kuwa sitokaa kwa muda mrefu wa kuishi Zanzibar kwa vile nina mipango yangu ya kurudi tena Tanzania bara hivyo kama miezi mitatu tu ntakuwepo hapa". Alisema Bushiri.
Katikati ya msimu uliopita Bushiri alichukua mikoba ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kujiunga na Mwadui FC ambapo aliikuta timu hiyo ipo nafasi ya tatu kutoka chini na kufanya kazi kubwa mpaka kuisadia kuinusuru kushuka daraja kabla ya kufutwa rasmi kazi mwanzoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.