Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Ziarani Nchini Cuba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa alipoondoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuelekea Nchini Jamuhuri ya Cuba kwa ziara maalum. Meya na Manispaa ya Wilaya ya Magharibi “B” Mstahiki Maabadi Ali Maulid  mwenye suti ya kijivu jivu akimtakia safari njema Balozi Seif katika ziara yake hiyo.

Na. Othman Khamis.OMPR. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Zanzibar leo asubuhi kupitia Mjini Dar es salaam kuelekea  Nchini Jamuhuri ya Cuba kwa ziara Maalum.


Balozi Seif  katika ziara hiyo ameondoka akifuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya wasaidizi wake kikazi. Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Balozi Seif aliagwa na baadhi ya Viongozi, Watendaji wa Serikali pamoja na Viongozi wa Vyama vya Kisiasa viliopo  hapa Nchini. Ziara ya Balozi Seif  Nchini Jamuhuri ya Cuba pamoja na mambo mengine itajumuisha  kutembelea Bunge la Nchi hiyo ambapo pia atapata wasaa wa kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chombo hicho cha juu cha kutunga Sheria.

Baadae  Ballozi Seif atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Elimu, Naibu Waziri wa Afya pamoja na kuona harakati za uzalishaji wa dawa katika Kiwanda cha Madawa cha Nchi hiyo sambamba na kufanya mazungumzo ya Ushirikiano wa pande hizo mbili. Zaiara hiyo ya Balozi Seif imelenga kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu ulipo kati ya Cuba na Zanzibar hasa katika Sekta ya Afya na Elimu ambazo zimeleta mafungamano ya Nchi hizo rafiki Kihistoria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.