Habari za Punde

Matukio ya Picha Mtaa Kwa Mtaa Zenj leo.

Vijana wakiwa katika usafiri wa gari ya ngombe katika kijiji cha Dunga Wilaya ya Kati Unguja wakiwa katika harakazi zao za kila siku kujipatia kipato kutokana kusafirisha mizigo kutoka eneo moja hadi jengine. Usafiri wa gari zinazotumika kwa kufutwa na ngombe ni moja ya usafiri katika vijiji vya Zanzibar.
Wananchi wakimfariji mtembea kwa miguu aliyogongwa na Pikipiki katika makutano ya barabara ya maisara na kikwajuni wakati akikata barabara hiyo na kupata majarahi ya kuchunika, ajali hiyo imehusisha pikipiki mbili kumgomba kijana hyu. mwenye shati jeupe akijifuta usoni. 


Maandalizi ya Ujenzi wa Maduka ya Kisasa yanayojengwa chini ya usimamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Zanzibar ZSSF , eneo hilo tayari limeaza kuzungushiwa uzio wa mabati kuaza kwa ujenzi huo baada ya kuondolewa wafanyabiasha wa eneo hilo maarufu kwa jina la makontena michezani.
Magari yakipita katika moja ya barabara ya michezani yakiwa yakikimbia mashimo yalioko katika barabara hiyo yaliochimbika kutokana mvua za masika zilizopita tayari baadhi ya barabara zimeshafanyiwa ukarabati wa kuweka lami katika mashimo hayo ili kuimarisha miundombinu ya barabara za maeneo mbalimbali ya Unguja yaliopata athari za mvua hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.