Habari za Punde

Rais Dk Shein azungumza na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na  Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar na Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar  katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji, [Picha na Ikulu.] 11 /08/2017.

  Baadhi ya Viongozi katika Benki ya Watu wa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kilichojumuisha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar[Picha na Ikulu.] 11/08/2017.
 Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar  alipokuwa kitoa maelezo ya Bodi yake wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ambacho kilichojumuisha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 11/08/2017.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohamed alipokuwa akichangia katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ambacho kimejumuisha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar na Bodi ya  Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar,(kulia) Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Fedha na Mipango Nd,Ali Khamis,[Picha na Ikulu.] 11/08/2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Nd, Juma Ameir alipokuwa akizungumza na kutoa ufafanuzi wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, ambapo Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) pia kimejumuisha Bodi ya  Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar,Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 11/08/2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.