Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Jamuhuri Makama Afungua Kongamano la 4 la Diaspora Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu akizungumza wakati wa hafla ya Kongamano la 4 la Watanzania Wanaoishi Nje Diaspora na kutowa nasaha zake kwa Wanadiaspora hao wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar na kufunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.
Wanadiaspora wakifuatila hutuba ya ufunguzi wa Kongamano hilo la 4 linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cleff Zanzibar.
Baadhi ya wadhamini wa Kongamano hilo la 4 la Watanzania Wanaoishi Nje Diaspora kutoka Mfuko wa Mafao wa PSPF wakifuatilia Kongamano hilo katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cleff Zanzibar.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia Ufunguzi wake katika Ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akihutubia na kutowa nasaha zake kwa Watanzania wanaoishi Nje Diaspora wakati wa Kongamano la Nne linalofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
WanaDiaspora wakifuatilia ufunguzi huo wa Kongamano la Nne la Kitaifa linalofanyika Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar.

MwanaDiaspora akiwa makini kumsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Yussuf Makamba akitowa nasaha zake kwao wakati wa Kongamano la Nne la Diaspora linalofanyika Zanzibar katika Hoteli ya Sea Ciff Zanzibar. 
Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakifuatilia Kongamano hilo la Nne la Diaspora wakati wa ufunguzi wake uliofanyika ukumbi wa hoteli ya sea cliff zanzibar mkoa wa kaskazini A Unguja. 

Mwakilishi wa Watanzania wanaoishi Nje Diaspora Asha Maulid akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Watanzania wanaoishi Nje Diaspora wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Diaspora lililoandalia na Idara ya Uhusiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.