Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Jangombe Wakombozi wa Ngwambu Warejea Zizini Kwao.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Taifa ya Jang'ombe "wakombozi wa ng'ambo" wamerejea kufanya mazoezi  katika uwanja wake wa nyumbani ulioko mtaa wa Taifa huko Mpendae ambapo mara ya mwisho kuutumia uwanja huo ilikuwa January mwaka huu.

Taifa walio chini ya kocha Saleh Maisara wamekuwa wakitumia Uwanja vya Mnazi Mmoja kama sehemu ya mazoezi kwa sababu ya ukubwa na uzuri wa uwanja huo tofauti na wa Taifa ambao upo karibu na makazi ya watu.

Imekua ni desturi kwa vilabu vingi hapa visiwani kwetu kubadilisha uwanja wa mazoezi baada ya kupanda ligi kuu kwa mfano Miembeni City fc wamekua wakitumia uwanja wa Amani kama sehemu ya kujiandaa na ligi kuu Zanzibar wakiachana na ule wa Miembeni Tumbaku.

Taifa wataendelea kuutumia uwanja huo kwa ajili ya kurejesha mashabiki wao na kupata radhi za wazee wa mitaa hiyo kwasababu timu hiyo sasa hivi imepoteza mashabiki na imani baada ya kutokufanya vizuri msimu uliopita katika hatua ya 8 bora.

1 comment:

  1. Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakatuh ndugu Othman, nikuulize, hizi habari unaposti mwenyewe au kuna watu wanapost kwa Niaba yako? Imekuwa ndio kawaida khasa kwa kuandika spelling mistakes, kila mada kama kufa lazima uone makosa ya mpaka umekuwa inatoa raha ya kusoma habari zako. Baya zaidi hii ni lugha ya kiswshili ambayo ndio lugha yetu rasmi, tumezaliwa nayo. Tujirekebishe.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.