Habari za Punde

Makundi ya Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Yawekwa Wazi Semtemba 20 KuazaNa: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 20, 2017 ambapo Makundi ya ligi hiyo tayari yameshawekwa hadharani huku jumla ya timu 27 zikigaiwa makundi mawili yani kundi A na kundi B.

Akizungumza na Mtandao huu  katibu wa ZFA Wilaya ya Mjini Yahya Juma Ali alisema ligi yao inatarajiwa kuanza Septemba 20 ambapo tayari makundi yameshaekwa hadharani huku wakihimiza vilabu vilivyokuwa havijalipa ada ya mashindano wajitahidi kumaliza ili waanze mashindano kwa amani na usalama.

"Ligi yetu ya Daraja la Pili tunatarajia kuanza Septemba 20, timu 27 tumezigawa makundi mawili, kubwa navisisitiza vilabu vilivyokuwa havijalipa ada ya Mashindano vifanye hima hima vilipe". Alisema Yahya.

Katika ligi hiyo kundi A kuna timu za Gulioni FC, Medson, Raskazone, FC Dira, Gulioni City, Mzalendo, Gereji, Hawai, Shangani, Urafiki, El Hilali,  Kijangwani, Small Renger na Kilimani Star.

Kundi B limejumuisha timu ya Kundemba, Amani Fresh, Magomeni, Muembeladu, Majimaji, Colombia, Kwalinatu United, ZMCL, Vikokotoni, Union Renger, West coast, Denger, Muembe makumbi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.