Habari za Punde

Jangombe Boys Hoi Kwa Timu ya Kilimani City Kwa Kukubali Kipigi cha Bao 1-0.

Mshambuliaji wa Timu ya Jangombo Boys Abubakary Mkubwa akimpita beki wa Timu ya Kilimani City Idrisa Zaidi wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Kilimani City imeshinda bao 1--0

MSHAMBULIAJI wa Kilimani City Bakary Nassor akimpita beki wa Timu ya Jangombe Boys Ibrahim Mohammed wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar

KOCHA Mkuu wa Timu ya Jangombe Boys Kwimbi akiwa na huzuni baada timu yake kukubali kipigo cha bao 1--0, dhidi ya Timu ya Kilimani City.
MSHAMBULIAJI wa Timu ya Jangombe Boys Hafidh Bakary na Beki wa Timu ya Kilimani City Thomas Peter wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Kilimani City imeshinda 1--0

 Timu ya Jang’ombe Boys imeendelea kufanya vibaya katika ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 na Kilimani city mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amaan.

Bao pekee la City limefungwa na Baraka Mashango dakika ya 19.

Mapema saa 8 za mchana Kiwanjani hapo Black Sailors wakaendelea na ari yao ya ushindi baada ya kuifunga Charawe mabao 2-1.

Mabao ya Sailors yamefungwa na Mustafa Hamad “Mboma” dakika ya 43 na Maulid Dhamiri wa Charawe alijifunga mwenyewe dakika ya 59 huku bao pekee la Charawe limefungwa na Boniface Afred dakika ya 45.

Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja itaendelea tena Alhamis ya Novemba 2, 2017 kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan  ambapo Saa 8:00 za mchana Mafunzo watakuwa na kazi kwa Kipanga na saa 10:00 za jioni JKU watakipiga na KVZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.