Habari za Punde

Kilele cha Mbio Za Mwenge wa Uhuru 2017 Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Viwanja vya Amaan Unguja.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akiwa na Viongozi wa Serikali wa SMT na SMZ wakisubiri kupokea Viongozi Wakuu wa Serikali katika viwanja vya Amaan kuhudhuria maadhimisho ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Amaan Zanzibar baada ya kumalizia mbio zake.Zanzibar.
Wananchi wa Visiwa na Unguja wakishangilia wakati wa kuwasili Viongozi wa Kitaifa katika Uwanja wa Amaan kuhudhuria maadhimishi ya Mbio za Mwenge Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Amaan Zanzibar kuhudhuria kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na viongozi wa Serikali alipowasili katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Amaan Zanzibar kuhudhuria Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizoadhimisha katika Mkoa wa Mjini Maghari Unguja. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Vijana wa halaiki na kuvisha kiskafu baada ya kuwasili katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Amaan Zanzibar leo.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghari Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakiwa katika viwanja vya Amaan Zanzibar baada ya kuwasili.     
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi ,Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jestina Mhagama kulia Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto.Zanzibar Mhe. Maudline Castico, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud. wakielekea jukwaa kuu. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakisimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. katika viwanja vya Amaan Zanzibar. 
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wakati wa sherere za Kilele cha Mbio za Mwenge zilizofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar leo asubuhi.
Viongozi wa Jukwaa kuu wakiwa wemesimama wakati wa kupigwa wimbo wa Taifa. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi ,Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jestina Mhagama kulia Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto.Zanzibar Mhe. Maudline Castico, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud. wakielekea jukwaa kuu. 



Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akisoma dua kuwaombea waasisi wa Serikali wakati wa Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika katika Viwanja vya Amaan Zanzibar leo. 

Father wa Kanisa Katoliki Zanzibar akisoma kuwaombea waasisi wa Muungano wa Tanzania wakati wa kilele cha mbio za mwenge katika viwanja vya Amaan Zanzibar.

Baba Askofu wa Kanisa la Mhunazini Zanzibar Micheal Hafidh akisoma Ibada ya kuwaombea waasisi wa Muungano wa Tanzania wakati wa sherehe za Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Amaan Zanzibar. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mohmoud akitowa salamu za Wana Mjini Magharibi wakati wa Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 zimeadhimishwa katika Mkoa wake.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi akihutubia wakati wa Kilele cha Mbio za Mwenge katika Mkoa wake wa Mjini Magharibi katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitowa taarifa za mbio za Mwenge wa Uhuru wakati wa maadhimishi ya mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar na kupokelewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.