Habari za Punde

Makocha Wilaya ya Magharibi A waanza kupigwa msasa


Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) leo kimefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa ngazi ya awali (Priminary) kozi ambayo imefanyika katika Ukumbi wa ZFA Wilaya ya Magharibi B Mwanakwerekwe Ijitimai.


Akifungua kozi hiyo Makamo wa Urais wa ZFA Unguja Mzee Zam Ali amewapongeza ZFA Wilaya ya Magharibi B kwa kuandaa kozi hiyo na amewataka washiriki kuendelea kujifunza zaidi ili Zanzibar watowe makocha bora.


“Nawapongeza ZFA Wilaya ya Magharibi B kwa kuandaa kozi hii nawapongeza sana, tena mukimaliza hii muendeleze tena kusoma mkufunzi bi Nassra ni hodari sana tunampongeza, nimefurahi washiriki wanatoa Wilaya tofauti na wengine mpaka Pemba nimefurahi sana nategemea tutatoa makocha bora”. Alisema Zam.


Nae mkufunzi wa kozi hiyo Nassra Juma ambae anatambulika Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) amesema kupitia kozi hiyo yatatokea mabadiliko makubwa na kuibuka makocha wazuri ambao watalisaidia soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.


“Kama watakuwa wasikivu katika masomo yao, naamini makocha hawa watalisaidia soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla”.

Jumla ya Makocha 31 kutoka Wilaya mbali mbali  wameingia katika Kozi hiyo ya siku 10 ambayo watafundishwa kwa nadharia na vitendo, kozi ambayo imeandaliwa na Chama cha Soka Wilaya ya Magharibi B.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.