TIMU ya Mwenge ya mji wa Wete, imeivuruga Chipukizi ya
mjini wa Chakechake, kwa mabao 2-0, kwenye mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kituo
cha Pemba, kwenye ngarambe iliopigwa uwanja wa FFU.
Mchezo
huo ulianza kwa kasi, na kila timu kuonyeshena ubabe wa kusakata soka, huku
wakitiwa hamasa na ari kupitia wapenzi na washabiki wao, waliojazana uwanjani
hapo.
Chipikuzi
walionekana kuwa wazuri, kwenye eneo la katikati, hivyo kuruhusu washambuliaji
wao, kufika mara kwa mara langoni mwa Mwenge, ingawa kisha mashuti yao kukosa
mwelekeo.
Mwenge
ukaanza kumwilika vyema, dakika ya 15 kwa bao la kuongoza, likifungwa na Abdu-l
Yussuf, baada ya walinzi wa Chipukizi, kufanya uzembe na kufungwa bao bilo.
Wanaume
wao waliokuwa wakiwinana vyema, walikwenda mapunziko, kwa wenyeji Mwenge,
wakiwa mbele kwa bao moja kibindoni, na ngwe ya lala salama, ilianza kwa kasi
mara dufu, huku timu zote, zikifanya mabadiliko.
Dakika
ya 80, Mwenge walijihakikisha ushindi wa pointi tatu muhimu, baada ya
mshambuliaji wake, alionekana kuitesa ngome ya Chipukizi Ali Salum, kuwapachika
bao la pili.
Kwa
matoke hayo, baada ya kila timu kushuka dimbani mara tatu, Mwenge ndio
inayoshika usukani wa ligi kuu ya Zanzibar kwa kituo cha Pemba, kwa kujikusanyia
alama tisa.
Timu
nyengine zinazokabana koo, kwenye nafasi ya pili ni Younger Islanders na FSC
zenye alama sita kila timu, huku timu za Okapi na New star zikiwa na pointi nne
nne, wakati timu za Chipukizi, Shaba na Kizimbani zikichuuana kwa pointi tatu
tatu.
Ligi
kuu ya Zanzibar kituo cha Pemba, itaendelea tena leo kwa mchezo mmoja tu, baina
ya Opec yenye point moja, watakaovutana
vilivyo na Kizimbani yenye point tatu, mchezo unaotarajiwa kuchezwa uwanja
pekee wa FFU Finya.
No comments:
Post a Comment