Habari za Punde

Wanawake wa Jumuiya ya JUWAMAKU Wafanikiwa Kuwarudisha Skuli Wanafunzi 120 wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kuendelea na Masomo yao ya Msingi na Sekondari.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake na Maendeleo ya Kuwahamasisha Wanawake katika Mkoa wa Kaskazini Unguja (JUWAMAKU) Bi.Mwanajuma Yussuf Mohammed, inayojishughulisha na kutowa Elimu kwa Wanawake wa Mkoa huo katika kazi za Maendeleo na kujikwamua na umasikini na kupambana na vitendo vya Udhalilishaji wa Watoto na Wanawake, akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusiana na changamoto wanazokumbana nazo na kufanikiwa kuwarejesha Watoto katika skuli za Mahonda na Donge kuendelea na masomo yao. Jumuiya hiyo inapata msaada kupitia TAMWA kupitia Mradi wa Canada Fund for Local Initiatives (CFLI) na Foundation for Civil Society (FCS) 
Mjumbe wa Jumuiya ya (JUWAMAKU) Bi.Fatma Ali Suleiman akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo na waandishi wa habari kufuatilia vitendo vya udhalilishaji wa Wanawake na Watoto katika Mkoa wa Kaskazini Unguja akielezea jinsi wanavyofuatilia kesi za udhalilisha katika vyombo husika na kupata ufumbuzi wa kesi hizo na watuhum,iwa kuchukuliwa hatua za kisheria.
Katibu wa JUWAMAKU Bi Hadia Ali Makame akikijibu maswali ya waandishi kuhusiana na jumuiya yao jinsi ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji katika Mkoa wao wa Kaskazini Unguja.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakifuatilia kwa makini mkutano huo na Wajumbe wa jumuiya hiyo changamoto wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao za kusaidia Jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.