Habari za Punde

Mawaziri wa Tanzania na Burundi Wafanya Ziara Katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo yaNdani na Mafunzo ya Uzalendo,Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Marco Gaguti, akizungumza katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo yaNdani na Mafunzo ya Uzalendo,Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea
Wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani)katika mkutano na wakimbizi hao, Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo yaNdani na Mafunzo ya Uzalendo,Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Mkimbizi wa Burundi anayeishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma Paul Ndalaizye., akitoa maoni kwa niaba ya wakimbizi wanaoishi katika kambi hiyo wakati wa Mkutano uliohutubiwa na NaibuWaziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo yaNdani na Mafunzo ya Uzalendo,Pascal Barandagiye(hawapo pichani), lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo yaNdani na Mafunzo ya Uzalendo nchini Burundi, Pascal Barandagiye(kulia), wakipiga ngoma baada ya kuwasili katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, iliyoko Wilayani Kasulu,mkoani Kigoma
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Marco Gaguti (kushoto), baada ya kuwasili Wilayani Kasulu,mkoani Kigoma  kwa ziara ya kikazi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.