Kaimu Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja ambae pia ni Mkuu wa Mkoa
Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema serikali imeweka mikakati
maalum katika kuhakikisha wanawafichuwa waovu ikiwemo udhalilishaji.
Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja
huko katika kiwanja cha Mpira Mkokotoni wakati akiendelea na ziara yake ya
kiserikali akiwa ni kusikiliza kero za wananchi zinazowakabili katika Wilaya
zao.
Alisema hatua hiyo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika
kupambana na vitendo vya udhalilishaji katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema Mkoa huo ni mkoa miongoni mwa vitendo hivyo licha ya
jitihada zinazochukuliwa na wanaharakati wa masulaya hayo ambayo mara nyingi
wamekuwa wanavikemea na kuvipiga vita.
Hata hivyo aliliagiza Jeshi la Polisi Mkoa huo kulitilia
mkazo suala hilo ikiwemo kufuatilia tatizo lilojitokeza hivi karibuni kwa mtoto
mwenye umri wa miaka mitano kufanyiwa kitendo cha kubakwa hakiwezi kuvumiliwa
ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa haraka.
Hivyo aliwataka wananchi kushirikiana na serikali katika
kuhakikisha wanakomesha vitendo hivyo ikiwemo kutoa taarifa kwa vyombo vya
sheria ili kuona vitendo hivyo vinaondoka kabisa katika mkoa huo.
“Hatupendi kuona kila wakati vitendo hivi vinatajwa midomoni
tu sisi linatusikitisha kupita kiasi kwani tunashangazwa kwa nini mkoa huu tu,
hivyo jitihada tuzifanye ili tuweze kukomesha kabisa” alisema.
Mbali na hayo aliwataka wazazi na walezi kuwa karibu na
watoto wao katika kufuatilia nyendo zao kwa lengo la kunusuru jamii na janga
hili ambalo limekuwa linatishia kuharibu vijana ambao ni taifa la baadae.
Akizungumzia dawa za kulevya Mhe.Ayoub alisema anahakikisha
wanafanya Operesheni maalum mkoani humo ya kukamata vikundi vyote vinavayojihusha
na uuzaji na usambazaji wa dawa hizo pamoja na watumiaji wa dawa hizo kwa
kuwachukulia hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment