NA ZUHURA JUMA, PEMBA
MWALIMU msaidizi wa
madrasa Seif Said Rashid ‘denja’ (18) mkaazi wa Kiungoni wilay ya Wete, anatuhumiwa
kumlawiti mwanafunzi wake, wa kiume miaka (9), wakati akiwa mtoni anakoga.
Baba mzazi wa mtoto huyo, alisema kuwa tukio hilo
lilitikea Oktoba 30 mwaka huu, ambapo mtuhumiwa alimlawiti mwanafunzi wake
huyo, baada ya kumkuta anakoga na kisha kumpeleka kichani, kumfanyia unyama huo.
Alisema kuwa, aliporudi kazini alipata taarifa kutoa kwa
mkewe wake kuwa, mtoto wao amekutwa akilawitiwa na mwalimu wake, ndio alipoanza
kumuhoji mtoto wake na kumueleza kuwa amemlawiti.
"Nilipoambiwa nilikasirika sana, siku ya pili
nilienda kituo cha Polisi Wete kuripoti, kisha tulienda hospitali ingawa
daktari alithibitisha kuwa hakuwahi kumlawiti“, alisema baba huyo.
Alieleza kuwa, alipomuhoji mtoto wake alimwambia kuwa
yeye alikuwa hataki na badala yake kutumia nguvu kumlazimisha na kumvua nguo
zote na ndio alipotaka kumfanyia, ingawa hakuwahi kutokana na kutokea watoto
wenzake katika eneo hilo.
"Kutokana na kishindo cha kukataa kitendo hicho
mwanagu, hakuwahi kumuingiza ndani kama alivyosema daktar, lakini alikuwa na
nia hiyo kwani alikuwa tayari kashamvua nguo", alieleza.
Mama mzazi wa mtoto huyo alieleza kuwa, alipata taarifa
kutoka kwa jirani yake, kwamba mtoto wake ameonekana kichakani na watoto
wenzake, akifanyiwa kitendo cha kulawiti na mwalimu wake wa chuoni ‘denja’.
"Nilipomdadisi mwanangu aliniambia kwamba yeye
alikuwa akikoga mtoni na ndio alipotokea mwalimu na kumkamata mkono, na
kumpelekea kichakani, ili amlawiti ingawa hakiufanikiwa”, alisema mama hiyo.
Kwa upande wake Khamis Hamad Nassor msaidizi wa sheria
aliwataka wazazi na walezi, kushirikiana katika malezi pamoja na kuchukua
juhudi ya kuwafuatilia, ili kujua sehemu wanazokwenda.
Nae Sheha wa shehia ya Kiungoni Omar Khamis Othman
aliwataka wazazi pamoja na mashuhuda wa tukio hilo, waache muhali na badala
yake, washirikiane pamoja katika kuhakikisha wanatoa ushahidi mahakamani.
Mratibu wa shehia hiyo, Mchanga said Hamad alisema kuwa,
mradi wa kukuza usawa wa Kijinsia na Kuwawezesha Wanawake GEWE ni mkombozi wa
Wanawake ba Watoto katika kuwaelimisha wanajamii kuviripoti vitendo vya
udhalilishaji.
Mkuu wa Dawati la kijinsia Wilaya ya Wete Khamis Simai
Faki alieleza kuwa, tayari kesi hiyo, imeshafika ofisini kwao na kwa sasa wanaendelea na uchunguuzi,
utakapokamilika hatua za kumfikisha mahakamani zitafuta.
Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete Haroub Suleiman Hemed,
alisema shehia ya Kiungoni ni moja ya shehia iliyopata elimu ya kupiga vita
vitendo vya udhalilishaji kupitia mradi wa GEWE, ingawa bado vitendo hiyo
vinatokea siku hadi siku.
Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Haji Khamis
Haji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Oktoba 30 mwaka huu saa 9:39 jioni,
huko Kiungoni Wilaya ya Wete Pemba.
Kamanda Haji alisema kuwa, tayari jalada la kesi hiyo
lishafunguliwa, ingawa mtuhumiwa bado hajapatikana, na kusema wapiganaji wake
kwa kushirikiana na raia wema wanamtafuta.
Kuanzia mwaka 2015 hadi mwezi Oktoba mwaka huu, tayari
wilaya ya Wete kumesharipotiwa matukio matukio 15 ya udhalilishaji kwa njia
utawiti ambapo matukio hayo ni yele yalioripotiwa Ustawi wa jamii pekee.
No comments:
Post a Comment