Habari za Punde

Taifa ya Jang'ombe na JKU yaipiku Yanga Zanzibar Heroes, zina wachezaji wanne Yanga watatu

TAIFA YA JANG’OMBE NA JKU YAIPIKU YANGA ZANZIBAR HEROES, ZINA WACHEZAJI 4, YANGA 3

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Taifa ya Jang’ombe na JKU zimeongoza kutoa idadi kubwa ya wachezaji ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) baada ya kutoa wachezaji wanne kila timu ndani ya kikosi hicho chenye wachezaji 30.

Wachezaji wanne wa Taifa ya Jang’ombe waliyoitwa katika kikosi hicho nahodha wao ambae ni mlinda mlango Ahmed Ali "Salula", mlinzi wa kati kinda Ibrahim Abdallah, kiungo Abdul Aziz Makame pamoja na mshambuliaji Ali Badru.

JKU ambayo nao wametoka idadi ya wachezaji wanne katika kikosi hicho yupo mlinda mlango wao Mohammed Abdulrahman "Wawesha", mlinzi wa kati Issa Haidar "Mwalala", kiungo Amour Suleiman "Pwina" pamoja na kiungo mshambuliaji Fesal Salum “Fei toto”.

Yanga imekama nafasi ya tatu katika orodha ya timu zilizotowa wachezaji wengi katika kikosi hicho ambapo imetoa wachezaji watatu akiwemo mlinzi wao wa kati Abdallah Haji "Ninja", mlinzi wa kushoto Haji Mwinyi Ngwali pamoja na mshambuliaji Matheo Anthony.

Jumapili iliyopita Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes),Hemed Suleiman (Morocco) alitangaza kikosi cha wachezaji 30 kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenji CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 hadi Disemba 9, 2017 nchini Kenya.

Kikosi kamili hicho:-
WALINDA MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe)
Nassor Mrisho (Okapi)
Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU)

WALINZI
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga)
Mohd Othman Mmanga (Polisi)
Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys)
Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar)
Haji Mwinyi Ngwali (Yanga)
Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege)
Issa Haidar "Mwalala" (JKU)
Abdulla Kheir "Sebo" (Azam)
Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe)

VIUNGO
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City)
Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe)
Mudathir Yahya (Singida United)
Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi)
Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar)
Amour Suleiman "Pwina" (JKU)
Mbarouk Marshed (Super Falcon)
Ali Yahya (Academy Spain)
Hamad Mshamata (Chuoni)
Suleiman Kassim "Selembe" (Majimaji)

WASHAMBULIAJI
Kassim Suleiman (Prisons)
Matteo Anton (Yanga)
Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe)
Feisal Salum (JKU)
Salum Songoro (KVZ)
Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys)
Mwalimu Mohd (Jamhuri)
Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.