Habari za Punde

YULE NYOTA ANAESAKWA NA SIMBA NA YANGA ATINGA MAZOEZI YA ZANZIBAR HEROES BAADA YA KUTOKA BENIN NA TAIFA STARS

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kiungo Mshambuliji wa Mtibwa Sugar Mohammed Issa "Banka" leo ameungana na wenzake kwenye mazoezi ya timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes).

Banka anakuwa mchezaji wa pili kutoka ligi kuu soka Tanzania Bara kujiunga na kikosi hicho akitanguliwa na mshambuliaji wa Majimaji Suleiman Kassim "Seleembe".

Sababu kubwa ya Banka kujiunga mapema na Zanzibar Heroes kumbe mchezaji huyo ana kadi za manjano 3 baada ya kupigwa kwenye michezo mitatu mfululizo akiitimukia timu yake ya Mtibwa hivyo mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumapili hii atalazimika kuukosa.

Mtandao huu umepiga stori na kiungo huyo kuhusu ujio wake Zanzibar Heroes ambapo amesema atapigana ili awemo katika kikosi cha mwisho.

"Hii ni mara yangu ya nne kuitwa Zanzibar Heroes lakini miaka yote huwa nachujwa sibahatiki kusafiri na timu kwenda kwenye Mashindano, lakini mwaka huu nataka kupigana ili nipate nafasi kwani Zanzibar kila ninaemuangalia ana uwezo mkubwa, kule Mtibwa nina kadi 3 za njano kwaiyo nimeruhusiwa kuja huku kwa vile sitocheza mchezo unaofuata". 

Aidha Banka pia amesema timu yoyote itakayomuhitaji na wakikubaliana atajiunga nayo lakini kwasasa bado ni mali ya Mtibwa.

"Mimi bado ni mchezaji wa Mtibwa na timu yoyote tukikubaliana sawa ila mimi ni Mtibwa bado na hakuna timu iliyonifata mpaka sasa" Alisema Banka.

Wachezaji ambao wanatokea ligi kuu soka Tanzania bara ambao bado hawajajumuika na wenzao ni Walinzi Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Viungo Mudathir Yahya (Singida United), pamoja na washambuliaji Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga) na Seif Rashid Abdallah “Karihe” (Lipuli).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.