Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (katikati), Akitoa Ushauri kwa Maofisa
Waandamizi juu ya umuhimu wa Utanuzi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, ili kukidhi ongezeko la wananchi
wanaofika kupata huduma mbali mbali za Uhamiaji Mkoani humo. Aliyasema hayo wakati
alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, Leo tarehe 15 Novemba, 2017.
Mrakibu
wa Uhamiaji, Gharib Saleh Suleiman (Kushoto), akitoa maelezo kwa Kamishna wa
Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (Kulia), kuhusu Utoaji wa Vibali vya
Ukaazi katika Kituo cha Uhamiaji, kilichoko ndani ya Mamlaka ya kukuza
Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika jana tarehe 14
Novemba, 2017. Kati kati ni Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji –ZIPA, Mrakibu Mwandamizi
wa Uhamiaji, Juma Sefu Juma.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, Akisisitiza jambo wakati akiongea
na Wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharib Unguja (hawapo
pichani), wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani hapo, Leo tarehe 15 Novemba,
2017. Kulia ni Kaimu Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharib, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Othman Khamis
Salum
Afisa
Uhamiaji Wilaya ya Magharib “B” Kamishna Mwandamizi wa Uhamiaji, Longido L.
Katovi, akitoa ufafanuzi kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud
Sururu, kuhusu uendeshaji wa Doria na Misako zinavyosaidia Udhibiti wa
Wahamiaji Haramu katika Wilaya zilizomo ndani ya Mkoa wa Mjini Magharib Unguja,
wakati wa ziara ya kikazi Mkoani humo, Leo
tarehe 15 Novemba, 2017.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, Akitoa Nasaha kwa Watumishi wa
Idara ya Uhamaiji, Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, kufanyakazi kwa mujibu wa
Sheria, Kanuni na Taratibu za kazi, Nidhamu, Weledi, Uwajibikaji na Utaoji wa
Huduma unaozingatia Maadili ya Kazi. Aliyasema hayo Leo tarehe 15 Novemba, 2017
wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo. Kulia ni Kaimu Afisa Uhamiaji
Mkoa wa Mjini Magharib, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Othman Khamis Salum na
Kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu wa Uhamiaji Zanzibar, Naibu Kamishna wa
Uhamiaji, Abullah Mbarouk Ramsa.
Wateja
waliofika kupata huduma za Uhamiaji katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini
Magharib Unguja, wakifurahia kauli iliyotolewa na Kamishna wa Uhamiaji
Zanzibar, Johari Masoud Sururu, kwamba Idara yake imejipanga kutoa Huduma bora
kama zilizivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Wateja. Aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya
kikazi Mkoani humo, Leo tarehe 15 Novemba, 2017.
umo, Leo tarehe 15 Novemba, 2017.
No comments:
Post a Comment