Habari za Punde

Finland Yaipatia Msaada wa Bilioni 75 Kuendeleza Misitu na Mafunzo ya Uongozi na Ubunifu.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) akionesha kalamu aliyozawadiwa na Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka (kushoto) ambayo imetengenezwa kwa mbao, akionesha uzalendo wa matumizi ya misitu. Kutoka kulia ni Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Mipango Bibi. Mary Maganga na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. John Rubuga.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James (kulia) akitia saini moja kati ya mikataba mitatu yenye jumla ya shilingi bilioni 75 kama msaada kwa Tanzania, Kushoto ni Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka kwa pamoja wakisaini mikataba hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) akibadilishana mkataba na Balozi wa Finland Bw.Pekka Hukka. Mkataba wa kwanza wa Euro milioni 9.9 ni kwa ajili ya kusaidia Taasisi ya Uongozi, wa pili wa Euro milioni 8.9 kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa ubunifu na watatu wa Euro milioni 9.5 ni kwa ajili ya program ya misitu.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) pamoja na Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka (kushoto) wakionesha moja ya mikataba mara baada ya kumaliza kutia saini mikataba hiyo.
Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja (Kulia) akiishukuru Serikali ya Finland kwa kuwapatia msaada wa Euro milioni 9.9 ambayo itawasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo. Kushoto ni Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (katikati, waliosimama mbele) akiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya hafla ya utiaji saini mikataba mitatu ya jumla ya shilingi bilioni 75. 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.