Habari za Punde

Historia Kujirudia? Zanzibar ilitwaa Kombe la CECAFA mbele ye Wenyeji Uganda 1995, Je itashinda Kesho dhidi ya Wenyeji Kenya?

Kikosi cha Zanzibar Heroes kilichoanza dhidi ya Uganda Cranes

Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.

Kesho ndio kesho fainali ya Ubingwa wa Kanda ya Afrika Mashariki na kati, maarufu Cecafa Senior Challenge Cup itapigwa saa 9:00 Alaasiri kati ya Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) dhidi ya wenyeji Kenya (Harambee Stars) mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya.

Zanzibar Heroes wametinga fainali baada ya kuwatoa mabingwa watetezi Uganda kwa mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali ya pili huku Harambee Stars waliwatoa Burundi kwa kuwachapa bao 1-0.

Zanzibar Heroes na Harambee Stars wote walitoka kundi moja A na walipokutana katika mchezo wao walitoka sare ya 0-0 mchezo uliopigwa Disemba 9 katika uwanja wa Kenyatta.

Historia inaonyesha Zanzibar imetwaa kombe hilo mara moja tu mwaka 1995 katika ardhi ya Uganda baada ya kuwafunga wenyeji Uganda bao 1-0 bao lililofungwa na Victor John Bambo, je na kesho watatwaa ubingwa huo mbele ya wenyeji Kenya?

Uganda ndiyo mabingwa wa kihistoria wa Mashindano hayo tangu mwaka 1971, wakiwa wamelitwaa mara 14, wakifuatiwa na Kenya mara sita, Ethiopia mara nne na Tanzania bara mara tatu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.