Habari za Punde

Mashindano ya Cecafa Kutimua vumbi kesho

 Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakijifua huko Machakos nchini Kenya wakijiandaa na kombe la Challenge. Mashindano yanaanza kesho

Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.
Mashindano ya CECAFA SENIOR CHALENJ CUP yataanza kutimua vumbi kesho nchini Kenya.

Wenyeji Kenya watafungua pazia hilo kwa mchezo wa kundi A dhidi ya Rwanda mchezo utakaopigwa majira ya saa 8:00 za mchana katika uwanja wa Machakos.

Saa 10:00 za jioni kesho kutakuwana na mchezo mwengine wa kundi A ambapo Tanzania Bara watacheza na Libya.

Michuano hii itafikia tamati Disemba 17, 2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.