Habari za Punde

Nusu Fainali Cecafa kupigwa kesho na Ijumaa

 Kikosi cha Zanzibar Heroes klilichoanza dhidi ya Libya
Kikosi cha Uganda Cranes


Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.

Nusu fainali za Mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup zinatarajiwa kupigwa kesho Alhamis ya Disemba 14 kati ya Wenyeji Kenya dhidi ya Burundi huku nusu fainali ya pili itasukumwa kesho kutwa Ijumaa ya Disemba 15 kati ya Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) dhidi ya Mabingwa watetezi Uganda.

Michezo yote hiyo itachezwa saa 9:00 za Alaasiri kwenye uwanja wa Moi hapa Kisumu nchini Kenya ambapo timu zote hizo nne tayari zimeshafika Mjini Kisumu kusubiri michezo hiyo huku mchezo wa fainali na wakugombea nafasi ya tatu itapigwa katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.

Kuelekea michezo hiyo ya nusu fainali tumefanikiwa kuzungumza na Nicholas Musonye ambae ni katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambapo amesema matayarisho yote yamekamilika kuelekea michezo hiyo huku akiipa tano Zanzibar.

“Nusu fainali zitachezwa Disemba 14 na 15, mpaka sasa matayarisho yote yanaendelea vizuri, Zanzibar nawapenda wanavyocheza na ningekuwa naruhusiwa kupenda timu basi ngependa Zanzibar”.Alisema Musonye.

Uganda “The Cranes” ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji hilo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali ilopigwa mjini Addis Ababa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.