Habari za Punde

Shirika la ZMCL Latiliana Saini Ushirikiano na Kituo Cha Utangazaji Cha CCTV Cha China

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZMCL) Muhammed Seif Khatib (kati kati kushoto) akiongoza mazungumzo ya ushirikiano baina ya Shirika hilo na Channel ya Televisheni ya China {CCTV) yaliyofanyika ukumbi wa Shirika hilo Mombasa ambapo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CCTV Li Yin (wa pili kulia) aliongoza ujumbe kutoka China.
 Mkurugenzi Mtendaji wa ZMCL Muhammed Seif Khatib akiwatembeza watendaji wa CCTV studio za kutangazia za Redio za shirika hilo kabla ya kutiliiana saini makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hzo mbili za utangazaji.
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CCTV  Li Yi (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa ZMCL Muhammed Seif Khatib wakitiliana sainai makubaliano ya ushirikiano baina ya vituo hivyo viwili vya utangazaji katika sherehe zilizofanyika Ofisi za ZMCL Mombasa Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZMCL Muhammed Seif Khatib akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CCTV  mara baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo mbili za utangazaji katika sherehe zilizofanyika Ofisini kwao Mombasa Mjini Zanzibar.

Picha na Ramadhani Ali Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.