Habari za Punde

Zanzibar Heroes yaingia Fainali CECAFA yaifunga Uganda Cranes 2-1

Kungo wa Uganda Allan Kaymbadde akifanya maarifa kumpita beki wa Zanzibar Heroes Abdallah Salum katika mchezo wa Nusu Fainali ya Cecafa. Zanzibar Heroes imeshinda 2-1 na kuingia fainali ambapo itapambana na Harambee Stars ya Kenya

Timu ya Taifa ya Zanzibar , Zanzibar Heroes imefanikiwa kuingia fainali ya CECAFA baada ya kuwaondoa mabingwa watetezi Uganda Cranes katika mchezo wa nusu fainali uliofanyuika Moi Stadium Kisumu, Kenya

Alikuwa ni kiungo Abdul aziz Makame aliyewainua wazanzibari dakiki ya 22 ya mchezo baada ya kuwafunga Waganda waliozemmbea kuokoa kona iliyopigwa .

Hata hivyo Uganda Cranes waliamka na kufanya mashambulizi dhidi ya Zanzibar na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 37 ya mchezo kupitia Derrick Nsibambi.

Hadi mapumziko timu hizi zilikuwa sare na hakuna mbabe.

Kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya kila pande hata hivyo ilikuwa ni Zanzibar iliyofanikiwa kupata goli la pili lililofungwa kwa njia ya Penelti na kiungo Mohammed Issa "Banka" katika dakika ya 57 ya mchezo .baada ya Joseph Nsubuga kumwangusha Ibrahim Hamad Hilika ndani ya kumi na nane. Joseph pia alilimwa kadi nyekundu

Ugandi ilizidisha mashambulizi lakini ngome ya Zanzibar ilisimama imara hadio mwisho wa mchezo.

Zanzibar Heroes itakutana na wenyeji Kenya Harambee Stars siku ya Jumapili katika mchezo wa fainali. Katika mchezo wa makundu timu hizi zilipokutana zilitoka sare ya kutofungana

Kila la kheri Zanzibar Heroes

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.