TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein leo Februari 4, 2018 anatarajiwa kuongoza Kikao Cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema Kikao hicho cha kawaida cha siku moja kitafanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi.
Kikao hicho ni cha kwanza tangu Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) walipochaguliwa kupitia Mikutano Mikuu ya Mikoa, Jumuiya na Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika mwaka jana katika Uchaguzi wa Chama.
No comments:
Post a Comment