Habari za Punde

Sekta binafsi Zanzibar yajadili mikakati madhubuti ya kufanikisha wiki ya Tanzania nchini Kenya

Waziri Wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum akizungumza katika ufunguzi wa mkutano na Wafanyabishara wa Zanzibar uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko tarehe 13 Aprili 2018. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hassan Khamis Hafidh na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Katibu wa Kamati ya Taifa ya maandalizi ya maonesho ya bidhaa za Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega.

Katika ufunguzi huo Mhe. Waziri Amina aliwasisitiza wafanyabiashara hao kushiriki katika maonesho pamoja na umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Diplomasia ya uchumi kwa vitendo. 
Balozi Anisa Mbega akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya maonyesho pamoja na kutoa ufafanuzi wa matukio mengine yatakayoambatana na maonyesho hayo kama vile kongamano la biashara, maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanzania. 
Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Saleh akiwahamasisha wafanyabishara kushiriki maonesho hayo pamoja na kuhakikisha wanafanya maandalizi ili kuweza kukamilisha vigezo na masharti ya ushiriki. 
Juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikiwasilishwa na viongozi. 
Sehemu ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano. 
Mkutano ukiendelea. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.