Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) Yapunguza Asilimia ya Riba Kutoka 18% Hadi 12% Kwa Wateja Wake Wanaochukua Mkopo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) Ndg. Juma Ameir Hafidh akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali viliko Zanzibar kuhusia na benki yake kupungua riba kwa wateja wake wanaochukua mikopo kwa kiasi kikubwa na kusema Wananchi na Wateja wa PBZ watanufaika na punguzo hilo na kutowa fursa Wananchi na Wafanyakazi wa Serikali kufaidika ba punguzi hili na kujikomboa na umasikini kwa kuweza kuwekeza katika maisha ya baadae.Mazungumzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Jengo la Bima Mpirani Zanzibar.  
Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali wakifuatilia taarifa hiyo kwa makini wakati wa mkutano wao na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Hafidh uliofanyika katika majengo ya Bima mpirani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Hafidh akitowa ufafanuzi kuhusiana na punguzo hilo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano wake na kusema PBZ kwa mwaka wa fedha imepiga hatua na kuongeza kwa faida kwa kiasi kikubwa.   
Maofisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) wakifuatilia taarifa hiyo wakati ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Hafidh katika ukumbi wa mkutano wa Makao Makuu uliopo katika majengo ya Shirika la Bima Mpirani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Hafidh akifuatilia maswali akiulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika makao makuu ya PBZ mpirani Zanznzibar kulia Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Bi. Khadija Shamte Mzee.
Mwandishi wa habari wa ITV na Redio One Ndg. Farouk Karim akiuliza swali kuhusiana na hatua hiyo ya PBZ kushusha riba kwa wateja wake wanapochukua mikopo kupitia PBZ.
Mwandishi wa Habari muandamizi Zanzibar Ndg. Issa Yussuf akiuliza suali kuhusiana na mikopo itkichefuchefu wakati wa mkutano huo na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidh, wakati wa mkutano huo wa kutowa mafanikio ya Benki ya Watu wa Zanzibar limited kwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.