Habari za Punde

Kampuni ya ndege ya Emirates yazindua ndege isiyo na madirisha

Kampuni ya ndege ya Emirates imezindua ndege ambayo imetengezwa na madirisha bandia
Badala ya abiria kuweza kuona nje moja kwa moja, sasa watalazimika kutazama picha kutoka nje wakiwa ndani kwa kutumia kamera za fibre-optic
Emirates inasema kuwa hatua hiyo inatoa fursa ya kuondoa madirisha yote katika ndege za siku zijazo, swala litakalozifanya kuwa nyepesi na kuongeza kasi yake.
Rais wa Emirates Sir Tim Clark amesema kuwa picha hizo ni nzuri sana ikilinganishwa na picha zinazotazamwa kwa macho.madirisha hayo bandia yanapatikana katika chumba cha kwanza cha ndege aina ya Boeing 777-300Er .
Sir Tim aliambia BBC lengo lao ni kuwa na ndege isiyo na madirisha kabisa.''Fikiria ndege isio na madirisha kabisa lakini unapoingia ndani kuna madirisha'', alisema.

Wasiwasi wa kiusalama

Wafanyikazi wa ndege wanatakiwa kuona nje ya ndege iwapo kuna dharura, mtaalam wa usalama wa angani Profesa Graham Braithwaite wa chuo kikuu cha Cranfield University alisema.
"Kuweza kuona nje ya ndege katika dharura ni muhimu, hususan wakati ambapo dharura ya uokoaji inafaa kutekelezwa'', alisema.
"Wahudumu wa ndege watalazimika kuona nje katika dharura , kwa mfano wakati wa moto, kabla ya kufungua mlango na kuanza uokoaji- na kitu chochote ambacho kitahitaji nguvu kufanya hivyo haitakuwa rahisi kuidhinishwa na afisa wa usalama wa angani''.
Hatahivyo maafisa wa usalama wa angani kutoka mamlak ya kudhitibi anga barani Ulaya European Aviation Safety Agency alisema: Hatuoni changamoto yoyote ambayo haiwezi kukabiliwa ili kuhakikisha kuwa kiwango cha usalama sawasawa na kile cha ndege ambayo ina madirisha ya wahudumu wa ndege.
Profesa Braithwaite alisema kwamba kizuizi kikuu katika ndege isiyo na madirisha itakuwa abiria wanavyohisi kuhusu teknolojia hiyo.

'Hakuna mbadala'

Mtaalam wa maswala ya usafiri wa anga John Strickland alisema kuwa ndege zisizo na madirisha zitakuwa na sauti ya chini. hatua hiyo pia itapunguza matumizi ya mafuta iwapo ndege hiyo itakuwa nyepesi.
"Chochote kitakachopunguza uzani wa ndege kitapunguza utumizi wa mafuta'', alisema.
Hatahivyo, yeye binafsi alipendelea kutaka kuona nje ya ndege : Napenda kuwa na madirisha , kwangu mie madirisha bandia ''sio mbadala''.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.