Habari za Punde

Korea Kaskazini na Marekani: Donald Trump na Kim Jong Un wakutana ana kwa ana Singapore

Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore.
Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili hao pekee na wakalimani wao.
Mkutano huo ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.Bw Trump amesema wawili hao walipiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka ya makubaliano.
Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.
Baadaye walitia saini waraka wa makubaliano.
Mkutano uliokua ukisubiriwa kwa hamu na ghamu ulifanyika katika Hotel ya Capella katika kisiwa cha utalii cha Sentosa.

Trump na Kim Jong-un wamekubaliana nini?

Mwandishi wa BBC amedondoa mambo manne makuu ambayo Trump na Kim wameafikiana kwenye waraka wao:
  • Marekani na Korea Kaskazini zitaanzisha uhusiano mpya wa Marekani na Korea Kaskazini kwa mujibu wa matamanio ya raia wa nchi zote mbili ya kuwa na amani na ustawi.
  • Marekani na Korea Kaskazini zitashirikiana katika kujenga na kudumisha amani ya kudumu Rasi ya Korea
  • Kukariri maafikiano ya Panmunjom ya Aprili 27, 2018 wakati wa mkutano wa marais wa Korea Kusini na Kaskazini, kwamba Korea Kaskazini itachukua hatua kuhakikisha kuangamizwa kabisa kwa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.
  • Marekani na Korea Kaskazini zimejitolea kuhakikisha kupatikana kwa mateka wa vita na watu waliotoweka vitani, pamoja na miili yao, ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwa wafungwa na miili ya wale waliotambuliwa.
  • Viongozi hawa wakiingia katika mkutano walionekana wenye tabasabu, na kusalimiana kwa kushikana mikono, na baadae Kim Jong Un alimshika bega Trumpa kisha wakaanza kuzungumza kwa msaada wa wakalimani wao.
Baadaye washauri na maafisa mbalimbali walitarajiwa kuingia kuendelea na mkutano huku suala la nyuklia likitarijiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana bado makubaliano yatakua yapi.
Akizungumza kabla ta mkutano , katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa umoja wa mataifa utatoa msaada wowote wa kuhamasisha makubaliono katika mkutano huo.
''Viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndio vinabaki kuwa lengo kuu, kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakua na changamoto za hapa na pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote," alisema Guterres.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.