Mwenyekiti
wa Bodi ya wakurugenzi wa TPB aliyemaliza muda wake Proffesa Lettice
Rutashobya akizungumza katika ufunguzi huo wa tawi kulia ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa TPB Sabasaba Moshingi
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa TPB Dkt Edmund
Mndolwa akizungumza katika hafla hiyo
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Sabasaba Moshingi akizungumza katika halfa hiyo |
Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses |
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB Dkt Edmund Mndolwa
amesema mtaji wa benki hiyo hivi sasa umekuwa kutoka Bilioni 8 hadi
kufikia Bilioni 60 hatua inayoonyesha utendaji mzuri wa wafanyakazi
kutokana na kutoa huduma bora zinazowafanya wateja kuvutiwa na kujiunga
nao.
Dkt Mndolwa aliyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa tawi
la Tanga la Benki hiyo lililopo eneo la Chumbageni Jijini Tanga ambao
ulifanywa na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Proffesa
Lettice Rutashobya kwenye halfa iliyofanyika mjini hapa na kuhudhuriwa
na viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa bodi ya wakurugenzi na
wafanyakazi.
Alisema hatua hiyo inatokana na huduma nzuri
inayotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo na hivyo kusaidia kuwepo kwa
ongezeko kubwa la wateja jambo ambalo limepelekea kuongezeka matawi
nchini kutoka 32 mpaka 74 kwa sasa.
“Niwapongeze sana TPB kwa
kasi kubwa ya utendaji mzuri mliokuwa nayo na kupelekea kuwezesha
kupanua wigo wa matawi kwa wateja wenu ambapo awali kulikuwa na matawi
32 lakini hivi sasa yamefikia 74 hii ni hatua nzuri sana hivyo kuwatake
muendelee nayo “Alisema.
“Lakini pia nimpongeze Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi anayemaliza muda wake Proffesa Lettice kwa kazi
nzuri aliyoifanya jambo ambalo limewezesha kufikia mafanikio yaliyopo
hivi sasa ndani ya benki hii nitaendelea kushirikiana na wafanyakazi
“Alisema.
Awali akizungumza katika halfa hiyo, Afisa Mtendaji
Mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshingi alisema benki yake imeendelea kukua
kwa kasi mwaka hadi mwaka na kupata faida ambayo imewezesha kutoa gawio
kwa serikali ya zaidi ya bilioni moja.
“Mwaka Jana 2017 benki
ilipata kiasi cha Bilioni 18.4 kama faida kabla ya kodi lakini pia
tumedhamiria kuboresha huduma zetu ili tuweze kufanya vizuri kwani
ushindani kwenye sekta hii ya mabenki ni mkubwa “Alisema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki
hiyo,Proffesa Lettice Rutoshobya alisema wanaamini tawi hilo jipya
litaongeza idadi ya wateja kwenye benki hiyo kwani lengo kubwa ni
kuwasogezea huduma karibu wananchi .
“Ni furaha kubwa sana kwetu
sisi TPB kuweza kufikisha huduma zetu hapa Tanga kupitia tawi letu hili
Jipya pia tunalo tawi lingine dogo kule wilayani Korogwe ambapo wateja
wetu wanapata huduma za kibenki”Alisema.
Naye Meneja wa TPB tawi
la Tanga, Mwajabu Mshana alisema mwitikio wa wakazi wa mkoa huu umekuwa
mzuri tangu walipoanza kutoa huduma zake maeneo hayo ya Chumbageni huku
akieleza wamejipanga kutoa huduma nzuri kwa wananchi (Habari kwa
Hisani ya Blog ya Kijamiiya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment