Habari za Punde

Mjumbe Wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mhe. Laila Burhan Ngozi Atembelea Majengo ya Baraza la Wawakilishi Chukwani leo.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberia Ali Maulid akizungumza na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bi. Laila Burhani Ngozi, alipotembelea Ofisi za Baraza na kuangalia jinsi ya Mkutano wa Baraza la Wawakilishi unavyoendesha na kujionea michango ya Wajumbe wakati wa Mkutano huo wa Kumi Baraza la Tisa la Wawakilishi linaloendelea kwa kupitisha Hutuba za Bajeti za Matumizi na Mapato ya Mwaka wa Fedha 2018/2019.

Mh Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM CC Lailah Burhan Ngozi akiwa ni mgeni wa Mh Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Maulid leo tarehe 04/06/2018 alipata fursa ya kwenda kusikiliza na kufatilia mijadala inavyoendeshwa.
Alipata kusikiliza Budget ya Wizara Ya Afya na jinsi serikali inavotekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Budget hii ilimgusa sana kwani alikuwa ni muajiriwa wa Wizara Hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.