Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Amefanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) na Wajumbe wa Tume.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Amefanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar na Wajumbe wa Tume leo.(ZEC)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu 119 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Kwa mjibu wa taarifa iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, ilieleza kuwa Katika uteuzi huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemteua Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Aidha, amewateua Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akiwemo Mabruki Jabu Makame, Feteh Saad Mgeni, Makame Juma Pandu,Dk. Kombo Khamis Hassan, Jaji Khamis Ramadhan Abdalla na Jokha Khamis Makame.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 20 Juni 2018 ambapo Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi wanatarajiwa kuapishwa siku ya Ijumaa tarehe 22 Juni 2018 saa 4 za asubuhi Ikulu Mjini Zanzibar.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.