Habari za Punde

Vijana Kisiwani Pemba Wakabidhiwa Vitendea Kazi.


AFISA Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Fatma Hamad Rajab, amewataka vijana kuwa na mashirikiano ya pamoja katika utekelezaji wa miradi wanayoiyanzisha, kwenye vikundi vyao vya ushirika, ili wazalishe bidhaa ambazo zitauzika katika soko la kibiashara ndani na nje ya Zanzibar.

Amesema vijana wengi hushindwa kuwa wazalendo na kujituma, katika utekelezaji wa miradi wanayoianzisha, hali inayopelekea  vikundi kukosa kuzalisha bishaa zenye ubora na kiwango kinachotakiwa.

Mdhamini Fatma ametowa wito huo, katika ofisi za wizara yake Gombani baada ya kukabidhi msaada wa charahani tatu, kwa kikundi cha Umoja na mshikamano cha Micheweni, Umoja ni nguvu cha Sizini, vifaa vya vespa kwa kikundi cha Vijana Bic cha gereji Mkoani na jezi seti moja kwa timu ya Polite FC ya Mkoani.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.